Numbers 12

Miriamu Na Haruni Wampinga Musa

1 aMiriamu na Haruni walianza kuzungumza dhidi ya Musa kwa sababu ya mke wake Mkushi, kwa kuwa alikuwa ameoa Mkushi. 2 bWaliuliza, “Je, Bwana amesema kupitia Musa peke yake? Je, hajasema kutupitia sisi pia?” Naye Bwana akasikia hili.

3 c(Basi Musa alikuwa mtu mnyenyekevu sana, mnyenyekevu kuliko mtu mwingine yeyote katika uso wa dunia.)

4Ghafula Bwana akawaambia Musa, Haruni na Miriamu, “Njooni katika Hema la Kukutania, ninyi nyote watatu.” Kwa hiyo wote watatu wakaenda. 5 dKisha Bwana akashuka katika nguzo ya wingu, akasimama kwenye ingilio la Hema, akawaita Haruni na Miriamu. Wakati wote wawili waliposogea mbele, 6 e Bwana akasema, “Sikilizeni maneno yangu: “Akiwapo nabii wa Bwana miongoni mwenu,
nitajifunua kwake kwa maono,
nitanena naye katika ndoto.

7 fLakini sivyo kwa mtumishi wangu Musa;
yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote.

8 gKwake nitanena naye uso kwa uso,
waziwazi wala si kwa mafumbo;
yeye ataona umbo la Bwana.
Kwa nini basi ninyi hamkuogopa
kuzungumza kinyume cha mtumishi wangu Musa?”

9 hHasira ya Bwana ikawaka dhidi yao, akawaacha.

10 iWakati hilo wingu liliinuka kutoka juu ya Hema, Miriamu akawa tayari ana ukoma, mweupe kama theluji. Haruni akamgeukia, akaona ana ukoma. 11 jKisha Haruni akamwambia Musa, “Tafadhali, bwana wangu, usituhesabie dhambi hii ambayo tumeifanya kwa upumbavu. 12 kUsimwache awe kama mtoto mchanga aliyezaliwa akiwa mfu, ambaye nusu ya mwili wake imeharibika hapo atokapo katika tumbo la mama yake.”

13 lHivyo Musa akamlilia Bwana akisema, “Ee Mungu, nakuomba umponye!”

14 m Bwana akamjibu Musa, “Je, kama baba yake angemtemea usoni, asingeona aibu kwa siku saba? Mfungie nje ya kambi kwa siku saba; baada ya hapo anaweza kurudishwa kambini.” 15 nKwa hiyo Miriamu akafungiwa nje ya kambi kwa siku saba, nao watu hawakuendelea na safari mpaka aliporudishwa kambini.

16 oBaada ya hayo, watu waliondoka Haserothi, wakapiga kambi katika Jangwa la Parani.
Copyright information for SwhKC